Msanii wa R&B wa Tanzania, Ben Paul ameonesha uwezo wake kwa mara nyingine katika jukwaa la muziki wa Kimataifa la Tamasha la Sauti za Busara usiku wa Februari 6, 2026, kwa kukonga nyoyo za mashabiki wake wa burudani ya muziki waliotoka kila pembe ya Dunia waliofurika uwanja wa Mnazi Mmoja, Unguja Zanzibar .
Kwa Ben Paul hii ni baada ya kupanda jukwaa la Sauti za Busara mwaka 2022, ilichukua miaka minne kwa Ben Paul, mtunzi wa Sofia, kurejea tena katika tamasha hilo jana Februari 6—mwonekano uliowarejesha mashabiki taratibu kwenye sauti iliyowahi kuashiria kipindi muhimu katika R&B
Amepanda jukwaani majira ya saa 4:40 usiku, na nyimbo zake mbalimbali, Alipitia nyimbo zilizopendwa na mashabiki, ikiwemo Maisha na Muziki, aliyoifanya kwa kushirikiana na Darassa.
Kwa kuingiza marejeo ya mitaa ya Zanzibar na maisha ya kila siku ya visiwani, Ben Paul aliibadilisha wimbo huo na kuufanya uwe wa karibu zaidi kwa hadhira ikiwemo kumpitisha 'Sofia' mitaa kadhaa wa kadhaa ndani ya Unguja ikiwemo Fordhani,
Aliwakumbusha mashabiki kuwa safari yake ilijengwa juu ya juhudi, si urithi: “Sitoki kwenye familia ya muziki,” amesema.
“Kila nilichofikia kimetokana na juhudi zangu mwenyewe za kufanya vizuri na kutengeneza muziki mzuri.” amemalizia Ben Paul.








0 Comments