Ruvuma
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imefanya ukaguzi wa kizimba cha mamba katika Kijiji cha Mtonya na Kituo cha askari katika Kijiji cha Nambecha, Wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma ikiwa ni miongoni mwa mikakati inayotekelezwa na serikali katika kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu.
Ukaguzi huo umefanyika tarehe 27 Februari 2026, ambapo watumishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, hususan Idara ya Wanyamapori kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya husika walitembelea maeneo hayo kwa lengo la kuona maendeleo ya miundombinu hiyo.
Kwa upande wa wananchi ambao ni wakazi wa maeneo husika walionesha furaha yao na kuipongeza serikali kwa juhudi za kuweka vizimba hivyo, ambavyo vimewasaidia kujikinga na madhara ya mamba pindi wanapotumia maji ya mto Mtonya kwa matumizi ya nyumbani. Aidha, wamekuwa wenye furaha, amani na kuona usalama wao kuimarishwa zaidi. Wananchi wameipongeza serikali kwa jitihada zinazofanyika.







0 Comments