Header Ads Widget

POLISI MBEYA WAPANDA MITI KUELEKEA FAMILY DAY YAO.

 

Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya familia ya Polisi mkoa wa Mbeya, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amewaongoza Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali kwenye zoezi la upandaji miti.

Zoezi hilo limefanyika Februari 12, 2026 katika eneo la Makao Makuu ya Polisi mkoa wa Mbeya Forest ya zamani jijini humo ambapo zaidi ya miche 100 ya miti imepandwa ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika suala la utunzaji wa mazingira na utekelezaji uoto wa asili.

Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Mazingira imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuhimiza utunzaji/uhifadhi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuhimiza upandaji miti na kutokata miti hovyo licha ya kwamba bado katika baadhi ya maeneo watu wamekuwa wakikata miti hovyo na bila kupanda mingine hatua inayohatarisha uhai wa misitu na mazingira kwa ujumla.

Pamoja na kufanyika kwa zoezi hilo katika makao makuu ya Polisi kimkoa, pia zoezi la upandaji miti limefanyika katika Wilaya zote za Polisi Mkoa wa Mbeya ikiwa ni maandalizi ya kuelekea siku ya maadhimisho ya siku maalum ya familia ya Polisi mkoa wa Mbeya (Police Family Day) inayotarajiwa kufanyika Februari 14, 2026, mfano ambao hauna budi kuigwa na watu wengine, taasisi na mtu mmoja mmoja ili kuhifadhi mazingira.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI