Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya kuboresha uchumi wa nchi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji leo ameshiriki semina ya kampeni ya kitaifa ya uhamasishaji uwekezaji wa ndani kwa lengo la kubadili fikra na mtazamo wa Watanzania kuhusu dhana ya Uwekezaji na kuongeza idadi ya wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi katika fursa mbalimbali za uwekezaji na hatimae kukuza uchumi wa nchi
sanjari na maono ya Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotekelezwa na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) kwa upande wa Nyanda za Juu Kusini iliyofanyika leo jijini Mbeya.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa semina hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Beno Malisa amewakumbusha washiriki umuhimu wa kuleta huduma za uwekezaji karibu na wananchi na kuhamasisha Watanzania kujitokeza kuwekeza na kueleza kampeni hiyo inalenga kubadili fikra kuhusu dhana ya uwekezaji,
kuongeza idadi ya wawekezaji kutoka ndani na nje, na kuleta maendeleo zaidi kwa taifa letu. Mbeya ni mkoa wenye milango mikubwa ya kibiashara kwa nchi za SADC, na fursa hizi zinapaswa kuzitumia kikamilifu.









0 Comments