Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Karatu kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wameendelea Kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo baina yao na jamii ya waadzabe
Akizungumza katika ziara iliyofanyika ya kutembelea jamii hiyo Mkuu wa Wilaya ya Karatu Dkt.Lameck Karanga amesema lengo ni kunifanya jamii hiyo kuweza kujihusisha na Utalii kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla.
Aidha Dkt. Lameck Karanga amewapongeza wananchi hao kwa kuendelea kudumisha mila na tamaduni za asili huku wakiwa kielelezo katika utunzaji wa amani na utulivu katika maeneo yao na kuwataka kuendelea kuwa kielelezo bora cha jamii nchini kwani serikali itaendelea kuwalinda na kuboresha shughuli za utalii katika eneo hilo.
Ameongeza kuwa serikali itaendelea Kuimarisha Utalii huyo kwa kuwawezesha makabila manne ambayo yanapatikana katika eneo la Jiopaki hiyo.
Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya jamii wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Joas Makwati amesema Jamii hiyo inayoishi lake Eyasi ni sehemu ya hifadhi ya Ngorongoro Jiopaki.
Ameleza kuwa mradi wa Jiopaki ya Ngorongoro unanufaisha jamii zinazokaa ndani na nje ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa kuwa Shughuli za ufugaji, uwindaji na kilimo hutegemea uwepo wa maji uhifadhi wa misitiu ya Ngorongoro.
Hata hivyo Makabila yote manne yanapatikana ndani ya jiopaki ya Ngorongoro Lengai inayopatikana wilaya ya Karatu, Ngorongoro na Monduli ,wilaya ambazo baadhi ya maeneo yake yanaunda jiopaki ya kidunia inayojulikana kama Ngorongoro Lengai Global Geopark inayotambuliwa na Shirika la Sayansi,Elimu na Utamaduni ( UNESCO).
Kabila la wahadzabe ambalo linaheshimika kutokana na mila na silka zake za kiasili linaamini kuwa nyama ya nyani ndiyo nyama bora na tamu kuliko zote duniani na limekuwa likimtumia mnyama huyo kama kielelezo muhimu kwa maisha yao huku kabila la wadatoga wakiendelea kutumia zana za kale katika uhunzi wa kufua bidhaa mbalimbali za kitamaduni.
Kabila la wahadzabe linaloishi pembezoni mwa eneo la Eyasi limekuwa likisifika kutokana na utaalam wake wakuchoma na kula nyama za nyani jambo ambalo limewafanya wageni kutoka ndani nan je ya nchi kuwatembelea ili kuona jinsi mnyama huyo alivyokuwa tunu kwa kabila hilo.









0 Comments