Header Ads Widget

MAREKANI YAISHAMBULIA VENEZUELA

 


Rais wa Marekani, Donald Trump amedai Taifa hilo limefanya shambulio kubwa Nchini Venezuela na kuwakamata Rais wake, Nicolas Maduro, na mkewe na kusafirishwa kwa ndege kutoka nchini humo

Kupitia chapisho lake kwenye mtandao wa Truth Social, Trump ameandika: "Marekani imefanikiwa kutekeleza shambulizi mkubwa dhidi ya Venezuela na kiongozi wake, Rais Nicolas Maduro, ambaye pamoja na mkewe, wamekamatwa na kusafirishwa nje ya nchi.


"Operesheni hiyo imefanyika kwa ushirikiano na Utekelezaji wa Sheria ya Marekani. Maelezo zaidi yatafuata. Kutakuwa na Mkutano na waandishi wa Habari leo saa 5 asubuhi, huko Mar-a-Lago. Asante kwa umakini wenu katika jambo hili" - ameandika Trump.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI