Header Ads Widget

BHANA NYANGUGE MTANDAO WASHEREHEKEA MWAKA MPYA KWA KUPANDA MITI 200.

 

Mwenyekiti wa Kikundi cha Bhana Nyanguge Mtandao, Mlanda Shigukulu (wa tano kushoto) akiwa ameshika mti kushiriki zoezi la upandaji miti uliofanyika Shule za msingi Nyanguge A, B na zahanati ya kijiji. (Picha na COSTANTINE MATHIAS).


Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


KIKUNDI Cha Bhana Nyanguge Mtandao ambao ni Wakazi na Wazaliwa wa Kijiji cha Nyanguge, wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, wameadhimisha sherehe za Mwaka mpya 2026 kwa kupanda miti zaidi ya 200 katika Shule mbili za msingi walizosoma pamoja na zahanati ya Kijiji chao.




KIKUNDI hicho kinaundwa na Wafanyabiashara, Watumishi pamoja na Wasomi waioshio nje ya Kijiji hicho, ambao wameadhimisha mwaka mpya kwa kupanda miti ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kurejesha uoto wa asili, kulinda vyanzo vya maji na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

WANANCHI wakishiriki kupanda miti 



Akizungumza na wanadishi wa habari, Makamu Mwenyekiti wa kikundi hicho, Motto Ng'winganele alisema kuwa wamepanda miti hiyo ili kuunga mkono jitihada za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za kurejesha Uoto wa asili na kuhifadhi Mazingira.

"Tumeadhimisha sherehe za Mwaka mpya 2026 kwa kupanda miti Shule ya Msingi Nyanguge 'A', Nyanguge 'B' pamoja za Zahanati ya Kijiji ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii kujenga utamaduni wa kupanda miti...miti ni agenda ya kitaifa na Taifa linahimiza tusiendelee kukata miti, tutumie nishati mbadala na sisi tumeanza kupanda miti ili iote kwa wingi" amesema Motto.


Makamu Mwenyekiti wa kikundi cha Bhana Nyanguge Mtandao, Motto Ng'winganele (kushoto) akipanda mti kwenye sherehe za Mwaka mpya katika Shule aliyosoma ya Nyanguge A, kulia ni Mwanafunzi mwenzake Mashala Sanagu.


Aliongeza kuwa katika Mkoa wa Simiyu miti imepungua sana hivyo wamefanya zoezi hilo ili kurejesha uoto wa asili na kurudisha Nyanguge iliyokuwa ya zamani yenye miti na misitu mingi.

Naye Masayi Sanagu mmoja wa kikundi hicho alisema kuwa wamepanda miti zaidi ya 200 na kila mwananchi aliyeshiriki zoezi hili amepatiwa miti miwili kwenda kupanda nyumbani kwake" amesema Masayi.


Mhasibu wa Bhana Nyanguge Mtandao, Masayi Sanagu (katikati) akipanda mti Shule aliyosoma ya Nyanguge A, kushoto ni Paskazia Majenga, kulia ni  Mwalimu Shota Mdege.


Mwalimu Said Said wa Shule ya Msingi Nyanguge A, aliwapongeza kikundi hicho kwa kupanda miti kwenye Taasisi za umma ili kurejesha uoto wa asili na kwamba miti hiyo itasaidia kupata kivuli, matunda na pia itakinga majengo ya serikali kuezuliwa na upepo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyanguge, Kija Kitanda alisema kupitia zoezi hilo la kupanda miti watahakikisha wanahamasisha wananchi kujenga tabia ya kupanda miti kwenye maeneo yao ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mwisho.


Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyanguge wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, Kija Kitanda akiongoza zoezi la kupanda miti lililofanyika siku ya mwaka mpya shule ya msingi Nyanguge A, B na zahanati.


























Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI