Makumbusho ya Taifa la Tanzania (NMT) imeshiriki katika zoezi la kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kushiriki upandaji miti kama ishara ya uzalendo na uwajibikaji wa kulinda mazingira.
Kupitia zoezi hilo, NMT kupitia kanda za Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kaskazini, na Kanda ya Mashariki wamepanda miti ili kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa utunzaji wa mazingira kama msingi wa maendeleo endelevu na uhifadhi wa urithi wa taifa.
Akizungumza wakati wakati wa zoezi hili Mkuu wa Kanda ya Mashariki Dkt. Gwakisa Kamatula amesema ĥatua hii inaakisi dhamira ya Makumbusho ya Taifa la Tanzania katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kulinda mazingira, kukuza uelewa wa jamii kuhusu uhifadhi wa maliasili na kuimarisha mchango wa sekta ya utalii katika maendeleo ya taifa.
“Uzalendo ni Kutunza Mazingira, Shiriki Kupanda Miti.”












0 Comments