Atimiza ndoto yake ya siku nyingi ya kuitembelea Tanzania
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) mapema leo Jijini Dar es salaam amempokea shabiki mashuhuri wa klabu ya Manchester City ya Uingereza Braydon Bent ambaye ametimiza ndoto yake ya siku nyingi ya kuitembelea Tanzania na kujionea vivutio mbalimbali ikiwemo Serengeti na Mlima Kilimanjaro.
Ni kama safari iliyochukua karne hivi ya kutoka tu Etihad Stdium hadi Serengeti! Shabiki huyo mtopezi wa Manchester City anasifika kwa kurekodi video akiongea Kiswahili na alipata kuahidiwa kuja Tanzania tangu mwaka 2020.
Leo, hatimaye, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi wametimiza ndoto ya shabiki huyo ambaye amepata pia kuwahoji mastaa kama Neymar, Aguero, Kocha Pep Guadiola na sasa akiwa mtangazaji wa mechi za Man City na pia akiwa na vipindi Sky News.
“Ilikuwa ndoto yangu kubwa kufika nchi hii nzuri. Kwa mapokezi haya naona kabisa tayari safari yangu imeanza vyema kabisa,” alisema Braydon akiwa ameambatana na Bw. Mark Bent, baba yake mzazi.
Karibu kwenye nchi bora kwa Utalii wa safari duniani.









0 Comments