Header Ads Widget

TANAPA IFTAR GALA: "KUENDELEA KUIMARISHA MAHUSIANO NA WATEJA, WADAU WA MAENDELEO NA JAMII"

 


"Mshikamano, Ukarimu, Umoja na kujali wengine katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan 


ARUSHA: Machi 18, 2026, Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) imeungana na wadau wa uhifadhi, na utalii, katika futari maalum iliyoandaliwa kuendeleza mshikamano na kujenga ukaribu na umoja katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla (Mkuu wa Mkoa wa Arusha) ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Joseph Modest Mkude.

Mhe Mkude ameipongeza TANAPA kwa kuendelea kudumisha utamaduni wa kuwakutanisha wadau wake na kushiriki nao katika shughuli zenye kugusa jamii, sambamba na mchango wake katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

TANAPA iliongozwa na Kamishna wa Uhifadhi Alhaji Musa Nassoro Kuji, ambaye alieleza kuwa futari hiyo ni sehemu ya utamaduni wa TANAPA kuendelea kujenga na kuimarisha mahusiano na wateja, wadau wa maendeleo pamoja na jamii kwa ujumla, hususan katıka kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan kinachosisitiza mshikamano, ukarimu, umoja na kujali wengine.

TANAPA imeendelea kudhihirisha nia yake ya dhati ya kuendelea kuwa karibu na wadau wake katika nyakatı zote.


Ramadhan Kareem.
















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI