Header Ads Widget

KAMISHNA MWISHAWA: USIMAMIZI WA VIHATARISHI NI NYENZO MUHIMU KUIMARISHA UTAWALA BORA


Na Calvin Katera - Manyara

Naibu Kamishna wa Uhifadhi anayesimamia Maendeleo ya Biashara Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Massana Mwishawa amefunga rasmi mafunzo ya usimamizi wa vihatarishi yaliyofanyika ukumbi wa Mikutano Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara yaliyoanza Januari 5, 2025 na kutamatika rasmi leo Januari 9, 2025.

Akizungumza katika zoezi hilo Kamishna Mwishawa amesema "Usimamizi wa vihatarishi ni nyenzo muhimu katika kuimarisha utawala bora, uwajibikaji na ufanisi wa taasisi. Katika mazingira ya sasa yanayobadilika kwa kasi, Shirika linawajibika na vihatarishi mbalimbali vya kimkakati, kiutendaji, kifedha, kimazingira na kiutawala".

Naye Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia Huduma za Shirika Abdallah Kiwango amesisitiza umuhimu wa Risk Champions kuishi na kutekeleza elimu ya usimamizi wa vihatarishi katika maandalizi ya mipango ya kimkakati, bajeti, utekelezaji wa majukumu ya kila siku, mifumo ya ubora (QMS) pamoja na ukaguzi wa ndani, ili kuongeza tahadhari dhidi ya matukio yajayo. 

 



Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi James Paschal na Mkaguzi wa Ndani (CIA) amesisitiza umuhimu wa mafunzo haya kuwa endelevu katika ngazi zote za usimamizi ili kuongeza uelewa wa pamoja na kuwezesha ugawaji bora wa rasilimali kwa kuzingatia vipaumbele. 

Kadhalika Mwakilishi wa Sehemu ya Mipango, ufuatiliaji na Tathmini  Afisa Uhifadhi Mkuu Bertiller Massawe amewakumbusha Risk Champions umuhimu wa kulisha taarifa katika Mfumo wa Usimamizi wa Vihatarishi wa Shirika (RIMS) ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihi kwaajili ya maamuzi. 

Mafunzo haya yamelenga kukuza ukomavu kwa Maafisa na Askari katika utekelezaji wa majukumu yao na yamejumuisha Maafisa Ishirini na Saba na Askari Watatu kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) pamoja na Mwezeshaji toka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI