Header Ads Widget

DODOMA YAUFUNGUA MWAKA 2026 KWA SHANGWE

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma


WAKAZI  wa Jiji la Dodoma wameukaribisha Mwaka Mpya 2026 kwa shamrashamra kubwa katika Uwanja wa Nyerere Square, ambapo maelfu ya wananchi walijumuika kusherehekea tukio hilo muhimu.

 Uwanja huo ulijaa furaha huku shughuli mbalimbali za burudani zikiendelea hadi usiku wa manane.

Sherehe hizo zilihusisha muziki wa wasanii wa ndani, ngoma za asili kutoka makundi mbalimbali pamoja na burudani nyingine zilizovutia umati wa watu wa rika tofauti.

Fataki zililipuka angani kuashiria mwanzo wa mwaka mpya, zikitoa mandhari ya kuvutia na kuupamba usiku wa jiji la Dodoma.

Shughuli nzima ilifanyika katika mazingira ya amani na utulivu, huku wakazi wakionesha mshikamano, furaha na matumaini mapya wanapoanza safari ya mwaka 2026.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI