Na Mariam Kagenda Kagera
Diwani wa Kata ya Bakoba Shabani Rashidi amefanya ziara ya kikazi pamoja na Maafisa kutoka Ofisi ya TARURA Bukoba, kwa lengo la kukagua na kubaini maeneo yenye uharibifu mkubwa wa barabara kwa ajili ya matengenezo ya dharura na maandalizi ya bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027.
Ziara hiyo ilihusisha barabara muhimu za Bishop Road/Gholani Street, Ukerewe Road pamoja na Shelisheli Road, ambazo ni muhimili mkubwa wa shughuli za kiuchumi, kijamii na usafiri wa wananchi wa Kata ya Bakoba na Manispaa ya Bukoba kwa ujumla.
Diwani Rashidi ameendelea kuonesha uongozi unaoshuka chini, kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana kwa karibu na taasisi za Serikali ili kuhakikisha changamoto za miundombinu zinapatiwa ufumbuzi wa haraka na wa kudumu. Hatua hii ni sehemu ya dhamira yake ya kuhakikisha Bakoba inaendelea kusonga mbele kimaendeleo.
Kupitia ushirikiano huu na TARURA Bukoba, maeneo korofi yameainishwa kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo ya haraka, sambamba na kuyaingiza kwenye mipango ya muda mrefu kupitia bajeti ijayo, ili kuboresha usalama, usafiri na mazingira ya biashara kwa wananchi.
Hatua hiyo inaendelea kujengwa juu ya misingi ya uwajibikaji, ushirikishwaji kwa vitendo








0 Comments