Header Ads Widget

AMANI YATAWALA, WATANZANIA WAKISHEREHEKEA MWAKA MPYA


Tanzania kama ilivyo kwenye Mataifa mengine kote duniani inasherehekea mwaka mpya wa 2026, Mamilioni wakishuhudia fataki, sherehe za kitamaduni na kidini na mikusanyiko ya kifamilia na kindugu, kuashirikia mwanzo wa mwaka mpya wa 2026 wakiwa na wingi wa matumaini ya ustawi na maendeleo yao binafsi.

Mkoani Dar Es Salaam, leo mchana katika maeneo mbalimbali kumeendelea kushuhudiwa mikusanyiko ya watu, ikiwemo eneo maarufu la Coco Beach, Wilayani Kinondoni ambapo watu wazima kwa watoto wameshuhudiwa wakibarizi katika fukwe hizo usalama ukiimarishwa na Polisi waliokuwa doria, kuhakikisha kila mmoja anaifurahia siku hii.

"Tunafurahi kuingia mwaka mpya, mwaka jana umekuwa na mchanganyiko wa mambo lakini tunamshukuru Mungu kwa hatua za maendeleo tulizopiga na zaidi kwa kuendelea kuitunza amani yetu. Niwaombe watanzania tusirudi tena kule kwenye vurugu, tuione thamani ya amani, tuilinde na tuwakatae wote wanaotaka kuipoteza." Amesema Bi. Amina Seleman, mmoja wa wananchi waliozungumza nasi Coco Beach.

Tofauti na wachache kwenye Mitandao ya kijamii walivyokuwa wakihamasisha kufanyika kwa maandamano hii leo, amani imeendelea kushuhudiwa, Watanzania wakipuuza miito hiyo ya maandamano na kuendelea na sherehe za mwaka mpya 2026.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI