Matukio Daima, Morogoro.
KATIKA oparesheni maalum ya kukabiliana na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limeteketeza shamba la bangi lenye ukubwa wa hekta 2.5 lililopo katika eneo la Mnyika, Kijiji cha Chonwe Kata ya Vidunda Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.
Wakati wa tukio hilo, Polisi walimkamata Festo Steven Maneno (30), huku taratibu za kumtafuta mmiliki wa shamba hilo zikiendelea kwa ajili ya hatua za kisheria.






0 Comments