Matukio Daima, Morogoro
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, ametembelea eneo la Iyovi wilayani Kilosa baada ya kifusi cha matope kuporomoka na kuziba sehemu ya barabara kuu ya Morogoro–Iringa.
Ameeleza kuwa mvua zinazoendelea ndizo zimechangia hali hiyo na ametoa tahadhari kwa madereva na watumiaji wa barabara kuchukua umakini mkubwa.
Baadhi ya madereva wakapongeza Jeshi la Polisi kufika eneo hilo kwa haraka ili kuzuia athari zinazoweza kujitokeza.







0 Comments