NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
IRINGA.
Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Iringa Dunstan Ndunguru amesema maadhimisho ya miaka 20 ya mahakama kuu ya iringa sio tu kumbukumbu ya historia bali ni fursa adhimu ya kutathimini walikotoka na wanakoelekea pamoja na changamoto wanazokutana na mafanikio katika tasnia ya utoaji haki tangu kuanzishwa kwa mahakama kuu kanda ya Iringa.
Jaji Ndunguru alisema hayo wakati akifungua mdahalo uliofanyika katika chuo kikuu cha iringa, kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 toka mahakama kuu kanda ya iringa ilipoanzishwa mnamo novemba 2005 ili kurahisisha upatikanaji na utoaji wa huduma za mahakama kuu kwa mkoa wa Iringa na Njombe.
Ndunguru alisema kuwa kanda ya kuanzishwa kwa mahakama kuu kanda ya Iringa wananchi wa Mkoa wa Iringa walilazimika kupata huduma ya mahakama kuu katika maeneo tofauti tofauti.
“Mkoa wa Iringa ulipata huduma ya mahakama kuu kutoka mahakama kuu kanda ya Songea,hivyo wanannchi waliokuwa wanahitaji huduma walitakiwa kusafiri kwenda Songea kupata huduma”alisema
“Baadae kutoka na umbali uongozi wa mahakama uliona ni vyema kusogeza huduma karibu na huduma zilihamishiwa Mbeya, hivyo wananchi waliendelea kusafiri kufuata huduma Mbeya”alisema
Alisema kuwa muhimili wa mahakama ukaona ni vyema kuanzisha huduma za mahakama kuu kanda ya Iringa na ndio 2005 huduma za mahakama kuu kanda ya iringa zilianzishwa.
“Maadhimisho ya haya sio tu kumbukumbu ya historia bali ni fursa adhimu ya kutathimini tulikotoka,tulikotoka, na wanakoelekea pamoja na changamoto wanazokutana na mafanikio katika tasnia ya utoaji haki tangu kuanzishwa kwa mahakama kuu kanda ya Iringa”alisema
Aidha alisema kuwa kwa Watumishi wa mahakama hiyo ni fursa ya kujipima kutokana na wananchi wanavyowaona katika majukumu yao ya kila siku.
“Sisis watumishi wa mahakama tupo tayari kupokea michango,ushauri na hoja mbalimbali zenye kulenga kutatua changamoto mbalimbali lakini pia kupata uelekeo katika siku zijazo katika utoaji wa haki ili kuhakikisha malengo yetu kama muhimili kwamba haki sawa kwa wote na mapema ipasavyo na kwamba watu wote wako sawa mbele ya sheria ili tuweze kufanikiwa ipasavyo”alisema Ndunguru.
Akizungumza wakati akitoa mada katika mdahalo huo kuhusu miaka 20 ya mahakama ya walikotoka na wanakoelekea Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu mkazi Iringa Joseph Manyama alisema kuwa mahakama imefanikiwa kupiga hatua katika kuboresha miundombinu ya majengo na matumizi bora ya Tehama ambayo yamethibiti upotevu wa majarada na nyaraka mbalimbali.
Manyama alisema kwa sasa mahakama ina mfumo pekee wa kusikiliza mashauri kwa njia ya kieletroniki,Pia Mahakama ina maktaba yakuhifadhia nyaraka mbalimbali pia imepunguza mrundikano wa mashauti katika mahakama zote za mkoa wa Iringa.
" Licha ya mafanikio lakini tunazo changamoto mbalimbali kama vile miundombinu chakavu hasa mahakama za Wilaya na Mwanzo pamoja na mfumo wa mashauri kutosomana" alisema
0 Comments