![]() |
| Marehemu Mzee Fabian Ngajilo |
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa anatarajiwa kuwa miongoni mwa viongozi wa Serikali pamoja na wananchi watakaoshiriki zoezi la kutoa salamu za mwisho kwa mwili wa marehemu Fabian Ngajilo, maarufu kama Mzee Sisi kwa Sisi, litakalofanyika kesho tarehe 1 Februari 2026 katika uwanja wa Samora mjini Iringa.
Kwa mujibu wa ratiba, zoezi hilo litafanyika katika Uwanja wa Samora, Manispaa ya Iringa, kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi, msemaji wa familia, Mwalimu Solomoni Mkangwa, amesema viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa pamoja na makundi tofauti ya kijamii wanatarajiwa kuhudhuria.
Ameeleza kuwa marehemu Mzee Sisi kwa Sisi, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 71, atazikwa katika Kijiji cha Ugwachanya, Kata ya Mseke, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, takribani kilometa 10 kutoka viunga vya mji wa Iringa.
Marehemu ni baba mzazi wa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Fadhili Ngajilo, na mfanyabiashara maarufu Fredy Vunjabei.






0 Comments