Matukio Daima -Mikumi
WATU watatu wamefariki Dunia na wengine watano kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria mali ya Kampuni ya ABC likitokea uelekeo wa Iringa kwenda Dar es salaam kupinduka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama alisema ajali hiyo ilisababishwa na dereva wa basi la ABC, Mussa Omary Mbaga (34),aliyedaiwa
kuyapita magari mengine kwa mwendo Kasi bila tahadhari kwenye kona kali na kugongana uso kwa uso na basi la Kelvan International lililokuwa linaelekea Songea
Kamanda Mkama alisema ajali hiyo iliyotokea usiku wa Novemba 23 katika eneo la Ng’apa, Mikumi ilisababisha vifo kwa watu watatu na majeruhi watano.
Aliwataja waliofariki Dunia kuwa ni Hawa Abdilahi Mohamed (28), Shire Abdil Shire (4) na Vaileth Mwaijembe (22-25).
Akasema majeruhi watano wa ajali hiyo wanaendelea kutibiwa hospitali ya St. Kizito Mikumi, huku dereva huyo akidaiwa kukimbia mara baada ya ajali na anatafutwa na Polisi







0 Comments