Na Shemsa Mussa -Matukio Daima
Kagera.
Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za Kaizirege na Kemebos zilizoko Manispaa ya Bukobamkoani Kagera, wamewaomba Watanzania hususani vijana kudumisha amani na utulivu na kutojihusisha na vurugu ili kuwawezesha wanafunzi kuepukana na wasiwasi na hofu hasa kipindi hiki ambacho wanafanya mitihani ya Taifa na ya kufunga mwaka.
Walitoa ushauri huo jana katika risala zao zilizosomwa na Jovan Mwandala darasa la saba na Innocent Madaraka Nyerere wa kidato cha nne katika mahafali ya darasa la saba na kidato cha nne ya shule hizo yaliyofanyika kata ya Ijuganyondo huku wakiaonyesha kusikitishwa na vitendo vya uvunjifu wa amani ambayo ni tunu ya Taifa letu.
"Tunawaomba wazazi wetu,kaka zetu,dada zetu,Watanzania wote kuendelea kudimisha amani na utulivu hari hiyo inatuondolea wasiwasi sisi na kutuongezea molali ya kusoma hasa wakati huu tunapoendelea na mitihani yetu ya Taifa ili tuweze kufanya vizuri katika mitihani yetu"alieleza Nyerere
Alisema kutokana na juhudi na jitihada zinazofanywa na Serikali,wazazi pamoja na uongozi wa shule za Kaizirege na Kemebos kuhakikisha wanafunzi hao wanapata ufauru mzuri inachangiwa na uwepo wa amani ambapo, humuondolea mwanafunzi wasiwasi na kumfanya asome kwa utulivu hivyo akaomba kila mtanzania kuunga mkono jitihada hizo.
Naye Jovan Mwandala alisema popote penye vurugu,vitisho na vita wanafunzi hawawezi kufanya vizuri hivyo ufaulu mzuri waliopata darasa la saba waliohitimu mwaka jana shuleni hapo walipata wastani wa alama 294.7 kati ya 300 ni kutokana na uwepo wa amani na utulivu ambapo husababisha walimu kufundisha kwa kujiamini na wanafunzi kusoma bila hofu.
Alisema alama hizo zinatokana na ufundishaji bora wa walimu wao,ushirikiano kati ya wazazi na uongozi wa shule uliojengeka katika misingi ya amani ya utulivu kutoka kwa waasisi wetu.
Mwalimu Kisha Ilamulira ni mkuu wa shule ya Shule hizo alisema uwepo wa shule zao katika Manispaa ya Bukoba na mkoa wa Kagera inachangia ongezeko la ajira,ulipaji kodi na kupanda kwa mapato utokanao na ulipaji kodi mzuri ambapo kwa mwaka 2024/2025 walibuka mlipaji bora wa kodi kwa mkoa wa Kageara.
Kwa upande wa mgeni rasmi Mussa Mwinyidaho ambaye ni mkuu wa kitengo cha biashara ndogo na za kati kutoka banki ya biashara (NBC) makao makuu aliyemwakilisha mkurugenzi mkuu wa banki hiyo Theobard Sabi aliwapongeza wazazi kwa kujinyima na kuwapeleka watoto wao shule ili kuwajengea urithi wao wa baadaye ambao ni elimu itayowasaidia kufauru katika maisha yao ya kesho.










0 Comments