Header Ads Widget

WATANZANIA WAASWA KUENDELEA KULINDA AMANI.


NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, amewataka watanzania wote kuendelea kulinda amani, umoja na mshikamano wa taifa, akisema hakuna nchi nyingine ya kukimbilia endapo amani ya Tanzania itapotea.

Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma, Kihongosi amesema amani ni rasilimali muhimu ambayo watanzania wanapaswa kuithamini na kuilinda kwa nguvu zao zote, huku akisisitiza kuwa taifa likipoteza utulivu, madhara yake huwa makubwa kwa wananchi, hususan watoto, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu.

Amesema wapo watu ambao, kwa madai ya maslahi binafsi, wanaendesha kampeni za uchochezi kupitia mitandao ya kijamii kwa kuhamasisha vijana na baadhi ya wananchi kufanya vurugu na kuvuruga utulivu wa nchi. 

"Nawaomba watanzania kuwakataa watu wa aina hiyo, kwa sababu wengi wao wanaishi nje ya nchi na kuwaacha vijana wa Tanzania kubeba mzigo wa madhara ya machafuko"

Aidha, Kihongosi amesema CCM  itasimamia kwa ukaribu kazi za serikali, akisisitiza kuwa serikali haitakisimamia tena chama kama ilivyokuwa ikielezwa na baadhi ya wachambuzi. 

Ameowaonya viongozi walioteuliwa serikalini wanapaswa kutimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwa chama kitafuatilia utekelezaji wa majukumu yao ili kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi.

MWISHO.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI