NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
DODOMA.Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, amesema kuwa ndani ya siku 11 tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alekiapo tayari 12,000 zilikuwa zimeshatangazwa.
Kihongozi alisema hayo leo Dodoma wakati akizungumza na vyombo vya habari kuwa hotuba ya Rais wakati akizindua Bunge imeweka wazi kasi ya utekelezaji wa maendeleo.
Kihongosi alibainisha kuwa ndani ya siku 11 tangu Rais Samia aapishwe, ajira mpya 12,000 tayari zimetangazwa zikiwemo ajira 7,000 za walimu na 5,000 za watumishi wa afya.
Kihongosi alisema hatua hiyo inaonysha serikali inatekeleza ahadi zake ndani ya siku 100 za kwanza, na ameeleza kuwa marufuku ya hospitali kuzuilia miili ya marehemu kwa sababu ya malipo imeanza kutekelezwa nchini kote, hatua ambayo Rais Samia aliwahi kuiahidi wakati wa kampeni na kuirudia mara kadhaa.
Aidha alisema kuwa" Leo nawatangazia rasimi kuwa, wajibu wetu kama chama cha mapinduzi ni kwenda kuisimamia serikali na si serikali kwenda kukisimamia chama"alisema
Akizungumzia hotuba ya Rais Samia aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa Bunge la 13 alisema ilikuwa ni hotuba ya kujenga umoja wa kitaifa, msamaha na mwelekeo mpya wa maendeleo kwa watanzania.
Kihongosi alisema hotuba hiyo iliainisha masuala mengi ya msingi kuhusu umoja, maadili, upendo na mustakabali wa taifa, akibainisha kuwa Rais Samia alisisitiza wajibu wa watanzania na viongozi kushirikiana katika kuijenga na kuilinda nchi.
Kihongosi alisema hotuba hiyo inaweza kuitwa hotuba ya ujenzi wa mshikamano kwasababu Rais Samia alisisitiza kuwa jukumu lake na la wabunge ni kuendeleza umoja wa kitaifa ili taifa liweze kupiga hatua katika maendeleo na kulinda hadhi ya Tanzania kimataifa.
alisema pia kwamba hotuba ya Rais Samia ilikuwa na ujumbe wa huruma na msamaha, kufuatia kauli yake ya kuomba vyombo vya sheria, hususani Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP), kuangalia uwezekano wa kuwasamehe vijana waliokamatwa kutokana na matukio ya vurugu za Oktoba 29, 2025.
Kwa mujibu wa Kihongosi, Rais Samia alieleza kuwa baadhi ya vijana walijikuta wakijihusisha na vurugu hizo kwa kufuata mkumbo, hivyo kama mlezi wa taifa ameonesha moyo wa huruma kwa kuwatakia msamaha.
MWISHO.







0 Comments