Header Ads Widget

CHAMA CHA MAPINDUZI KUWASHUGHULIKIA WATENDAJI WAZEMBE


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima Media Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuwa kitachukua hatua kali dhidi ya viongozi wote wazembe na wanaojihusisha na vitendo vya rushwa, kikisisitiza kwamba hakitavumilia kiongozi yeyote anayeshindwa kuwajibika kwa wananchi. 

Akitoa kauli hiyo jijini Dodoma, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenan Kihongosi, amesema chama kitaweka vipimo maalum vya kupima utendaji wa viongozi katika ngazi zote ili kuhakikisha uwajibikaji unazingatiwa kikamilifu.

"Mawaziri na Manaibu Mawaziri walioteuliwa na Rais wanapaswa kwenda sambamba na kasi ya utendaji ya kiongozi wa nchi, akibainisha kuwa ingawa baadhi yao ni wapya na wanafurahia uteuzi, wanapaswa kufahamu kuwa Rais anataka kazi yenye matokeo kwa wananchi na hana mzaha katika masuala ya utumishi wa umma., "

Amesisitiza kuwa CCM haitasita kumchukulia hatua yoyote atakayekwenda kinyume na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Kihongosi amesema chama kipo bega kwa bega na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kuimarika nchini.

 Amewapongeza pia viongozi walioapishwa akiwemo Rais wa Zanzibar, Dot, Hussen Mwinyi,Dkt,Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Fedha, Mwiguru akiwataka kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu na kuwatumikia wananchi kwa weledi.

Akizungumzia hatua ya Rais Samia ya kuomba vijana waliokamatwa kwa vurugu za Oktoba 29 waachiwe, Kihongosi amesema ni uthibitisho wa uongozi wa huruma na busara. Pia ametoa pongezi kwa uundwaji wa timu maalum ya kuchunguza vurugu hizo pamoja na ahadi ya Rais kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya ndani ya siku 100.

Kihongosi amesema kuwa ndani ya siku 11 ajira zimeanza kutolewa na hospitali zimekatazwa kutoza malipo yasiyo rasmi has a suala la kutuza maiti fedha huku akiksisitiza wananchi wanapaswa kupata huduma stahiki bila usumbufu.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI