Wananchi wa Mkoa wa Dar Es salaam wameeleza athari kubwa za kiuchumi wanazokumbana nazo kwasasa katika baadhi ya maeneo kutokana na kukosekana kwa usafiri wa mabasi yaendayo haraka maarufu kama Mwendokasi, wakiiomba serikali kuharakisha upatikanaji wa huduma ya usafiri huo muhimu.
Wananchi hao akiwemo Pius Focus, ameeleza kuwa kwasasa hali ya usafiri imekuwa ya shida kutokana na gharama kubwa za nauli zinazotokana na kupanda magari zaidi ya mawili katika umbali waliokuwa wakisafiri kwa Basi moja la mwendokasi, huku pia msongamano mkubwa wa magari ukiwachelewesha katika shughuli zao za kiuchumi na Kijamii.
Wameeleza pia kero yao ya nauli za daladala na Bajaji kupandishwa tofauti na awali kutokana na mahitaji ya Vyombo hivyo vya usafiri kuongezeka, wakisema suala hilo limewafanya kutumia fedha nyingi kwenye kulipia gharama za usafiri.
Wananchi hao wametoa wito kwa serikali kuurejesha usafiri huo kwa wakati ili pia kuondoa kero ya msongamano mkubwa wa magari barabarani, kutokana na kuwafanya hata waliokuwa wamepaki magari yao ndani kuanza kutumia magari hayo kutokana na kutatizika kwa usafiri wa mabasi hayo ya mwendokasi.








0 Comments