Zawadi Matuku, Mfanyabiashara wa Chanika kwa Ngwale Mkoani Dar Es Salaam ameishukuru serikali na Vyombo vya ulinzi na usalama kwa udhibiti wa amani na utulivu nchini, akisema kilichotokea wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 hakuwahi kukizoea kwani Tanzania inasifika kwa amani na utulivu kote duniani.
Matuku ameyasema hayo wakati akieleza uzoefu wake dhidi ya uvunjifu wa amani uliojitokeza, akisema kwamba aliamini siku hiyo ya upigaji kurwa ungekuwa wa amani na wafanyabiashara wangeendelea na shughuli zao kama kawaida baada ya kupiga kura.
Ameomba suala hilo kutokujirudia tena, akiwahamasisha Vijaba kujiepusha na mikumbo na kuwataka kutumia muda wao mwingi katika kujiendeleza kiuchumi na kusimamia ustawi wa maisha yao badala ya kutumika na makundi yasiyoitakia mema Tanzania.






0 Comments