Header Ads Widget

TUIENZI NA KUILINDA AMANI YA NCHI YETU- WAJASIRIAMALI


Vijana wajasiriamali kutoka Mkoa wa Dar Es Salaam wametoa wito kwa Vijana wengine nchini kuienzi na kuilinda amani ya Tanzania na kujiepusha na ushawishi na makundi yenye kuwahamasisha kufanya vurugu na kuharibu amani, umoja na mshikamano wa Watanzania.

Wito huo umetolewa majuma kadhaa baada ya vurugu na uharibifu wa Jumatano ya Oktoba 29, 2025 ambapo kwa nyakati tofauti katika Miji ya Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Songwe kulitokea makundi ya watu waliokuwa wakiiba, kuharibifu na kuchoma moto mali mbalimbali za umma na za binafsi katika maeneo hayo.

Miongoni mwa waliozungumza nasi ni pamoja na Akinamama wanaofanya biashara ya chakula maarufu kama Mama ntilie, ambapo mbali ya kueleza athari za kiuchumi, Bi. Asha Mbaraka amesisitiza kuhusu amani na akiiomba serikali kushughulikia tatizo la mfumuko wa bei za bidhaa za chakula nchini.

Aidha Vijana wengine pia wamesisitiza umuhimu wa kulinda amani na kupunguza mihemko kwa Vijana, wakisema kile ambacho kilitokea Oktoba 29, 2025 haikuwa maandamano bali vurugu, ghasia na uharibifu wa mali na huduma za kijamii.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI