Na Ester Sebastian (UOI) Matukio Daima Media.
Baadhi ya vijana kutoka mtaa tofauti tofauti katika Mkoa wa Iringa wameeleza changamoto ya rushwa kwa vijana wa maskini kukosa Ajira na kusababisha maendeleo katika jamii.
Akizungumza na Matukio Daima, Michael Likeleka amesema maisha ya sasa ni changamoto sana kwa vijana masikini kwasababu kijana wa masikini unaweza ukamaliza chuo na una ufaulu mzuri lakini kutokana na umasikini unashindwa kupata kazi kutokana na rushwa.
Amesema changamoto za rushwa hupelekea mtu kuingia kwenye ajira kwa kinyonge kwasababu mfanya kazi hufanya kazi kwa kunyonywa anapata mshahara mdogo kwasababu bosi anataka kila mwisho wa mwezi amlipe bosi nusu ya mshahara wake.
"Vijana wa maskini ni ngumu kupata kazi kwaajili ya rushwa na kama ukipata kazi basi kwa vipengele vingi yaani unaweza kupata kazi bosi kupitia ule ule mshahara wako unaoupata atataka akulipe nusu kwa sababu ya rushwa" Alisema Likeleka
Mkazi wa Tumaini Sharif Abdallah amesema kijana wa maskini unaweza ukapata kazi Bosi anataka kulala na wewe ili upate kazi na vijana wengi wakimaskini unakubali kulala na Bosi wako ujui anamadhara gani hupelekea mtu kupata magonjwa na kupelekea kifo.
"Bosi anaweza akataka ulale nae ili haweze kukupa kazi kwasababu ya umaskini mtu unakubali kutoa rushwa la kingono Bosi wako ili upate kazi na mwisho wasiku kupata magonjwa nakupelekea kifo" Alisema Abdallah
Mkazi wa Country side Denister Mahengo amesema napenda kuishauri Serikali hiwe macho hususani maswala ya rushwa maana husababisha ubaguzi kwa vijana maskini na kudidimiza maendeleo katika jamii
"Rushwa ni changamoto kwa vijana maskini kupata kazi kwaiyo ningependa kushauri Serikali ya awamu ya sita hiwe macho na kutokomeza rushwa katika nchi yetu ili vijana maskini waweze kupata haki kama vijana matajiri ili usawa uwe kwa wote maskini na matajiri" Alisema Mahengo







0 Comments