Header Ads Widget

MKURUGENZI WA MANISPAA YA KIBAHA ATOA WITO KWA JAMII KUTUNZA MIONDOMBINU YA MAENDELEO


Kibaha, Tanzania – Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Rogers Shemwelekwa, amewataka wananchi wa Manispaa hiyo kutunza miundombinu na miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ili kuendana na kasi ya maendeleo ya serikali.

Dkt. Shemwelekwa ametoa wito huo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika Kata ya Mbwawa, ambapo amesisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu katika kuilinda na kuitunza miradi inayotekelezwa kwa manufaa yao.

“Haipendezi kuona serikali inatoa fedha nyingi kutekeleza miradi ya maendeleo lakini wananchi hawatunzi miundombinu hiyo,” alisema Dkt. Shemwelekwa. “Kwa mfano, Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha imetoa shilingi milioni 420 kwa ajili ya kutengeneza barabara zenye lengo la kuboresha huduma kwa wananchi, lakini changamoto kubwa imekuwa wananchi kutokutunza barabara hizo mara baada ya kufunguliwa.”


Ameongeza kuwa ni muhimu kwa wananchi kutambua kwamba miradi ya serikali ni matokeo ya kodi zao, hivyo ni wajibu wao kuilinda na kuhakikisha inadumu kwa muda mrefu.

 “Kama leo tumefungua barabara, basi mwaka ujao tuweke kifusi na kuendelea kuboresha zaidi, ili tuendelee kupiga hatua za kimaendeleo,” alisisitiza.

Kwa upande wao, wananchi wa Kata ya Mbwawa wamempongeza Dkt. Shemwelekwa kwa utendaji wake na kasi ya kusimamia maendeleo, wakisema kuwa anatekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kutatua changamoto zinazowakabili.

 Wameahidi kuendelea kumpa ushirikiano ili kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inafanikiwa na kuleta manufaa kwa jamii.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI