Na Shemsa Mussa -Matukio Daima
Kagera.
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Mkoani Kagera imetimiza ahadi ya mashine ya urudufishaji (Photocopy )iliyoghalimu kiasi Cha Milion 4 Katika Shule ya msingi kashai.
Akizungumza katika makabidhiano hayo mwalimu Mkuu Wa Shule hiyo Bi,Eliena paulo amesema Shule hiyo ilikuwa na changamoto ya urudufishaji hasa katika kipindi Cha mitihani.
Mwalimu Mkuu Wa Shule ya kashai,,Eliena pauloPia Mkuu huyo ameishukuru TRA kwa kutimiza ahadi yao, akieleza kuwa mashine hiyo itaondoa usumbufu waliokuwa wakipata katika kuchapisha mitihani na nyaraka muhimu. Amesisitiza kuwa vifaa hivyo vitatunzwa vizuri ili viendelee kutoa huduma inayotarajiwa.
Meneja Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kagera imekabidhi mashine ya photocopy yenye uwezo wa ku-scan na kuchapisha (printer) katika Shule ya Msingi Kashai, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi iliyotolewa wakati wa mahafali ya darasa la saba mwaka huu. Tukio hilo limefanyika katika eneo la shule hiyo iliyopo Manispaa ya Bukoba, Kata ya Kashai Leo Nov. 25 Mwaka huu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Meneja wa TRA Castro John amesema kuwa msaada huo ni miongoni mwa jitihada za Mamlaka katika kurudisha kwa jamii na kuunga mkono maendeleo ya elimu nchini. Amesema TRA ni ya wananchi na inaliona jukumu la kusaidia maendeleo ya sekta mbalimbali, ikiwemo elimu.
Aidha, aliwahimiza wazazi na wafanyabiashara kuendelea kulipa kodi kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kupeleka huduma muhimu katika maeneo mbalimbali kwenye jamii.
Nae Afisa elimu Wa kata hiyo Frederick Musinga ametoa pongezi kwa mamlaka hiyo Kwa kuiona Shule hiyo na kuwa nyenzo hiyo itawasaidia walimu pamoja na wanafunzi Kwa ujumla Katika Shule hiyo.
Kwa niaba ya wazazi Bw Elick Edwin amesema Kwa kilichofanywa na mamlaka hiyo ni njia Moja wapo ya kuona umuhimu Wa kulipa Kodi na kuwasisitiza wazazi kulipia kodi bila usumbufu wowote.
Naye John Paul, Kaka Mkuu wa shule, ameishukuru kwa niaba ya wanafunzi akisema kuwa mashine hiyo itachangia kuongeza ufaulu kwani itarahisisha maandalizi ya mitihani na nyaraka za kujifunzia.
Utekelezaji wa ahadi hiyo umeendelea kuonesha dhamira ya TRA katika kuiwezesha jamii kupitia uwajibikaji na uboreshaji wa mazingira ya elimu nchini.





0 Comments