Header Ads Widget

TMDA YAANZA VYEMA MOROGORO MASHINDANO YA SHIMMUTA 2025


Morogoro, — Timu za Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) zimeanza kwa ushindi mzuri katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Taasisi za Umma (SHIMMUTA) 2025 baada ya kufanya vyema katika michezo ya mpira wa miguu na netiboli.

Katika mpira wa miguu, TMDA iliibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya DIT. Bao pekee la mchezo lilifungwa na James Tanguye, na kuihakikishia TMDA pointi tatu muhimu katika hatua ya makundi.

Katika netiboli, TMDA iliendelea kung’ara kwa kuichapa TPHPA kwa alama 40–15, ushindi uliodhihirisha maandalizi na ubora wa kikosi hicho.

Mafanikio haya ya mwanzo ni ishara ya dhamira ya TMDA kufanya vizuri katika mashindano ya mwaka huu na kuendeleza rekodi nzuri katika michezo ya taasisi za umma.

TMDA inaendelea kuwakaribisha wafanyakazi, mashabiki na wadau kuendelea kuiunga mkono timu zao katika michezo inayofuata.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI