Header Ads Widget

TMDA QUEENS YANG'ARA MOROGORO KWENYE MASHINDANO YA SHIMMUTA 2025


Morogoro, — Timu ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)upande wa Netiboli TMDA QUEENS imeanza kwa ushindi mnono wa 40 kwa 15 dhidi ya timu ya TPHPA katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Taasisi za Umma (SHIMMUTA)2025 katika viwanja vya Magadu mjini Morogoro.

Ushindi huo unadhihirisha maandalizi na ubora wa kikosi hicho cha TMDA QUEENS.

Mafanikio haya ya mwanzo ni ishara ya dhamira ya TMDA kufanya vizuri katika mashindano ya mwaka huu na kuendeleza rekodi nzuri katika michezo ya taasisi za umma" Imebainisha taarifa ya TMDA.

TMDA inaendelea kuwakaribisha wafanyakazi, mashabiki na wadau kuendelea kuiunga mkono timu zao katika michezo inayofuata.

"Mchezo huu kwetu ulikuwa na malengo ya: Kuzingatia maelekezo ya mwalimu,  Kurudisha fitness na kujenga chemistry,

Lakiki pia Burudani; Yes! Kwetu sisi haya yalikuwa mazoezi na kujenga mbinu mpya, Leo tumeshuhudia Dada Husna na Halima wakisusiana kushinda (yaani kampa kampa tena).

Ahsanteni sana QUEENS, kituo kinachofuata  waajiandalie wao, sisi hatushuki mpaka tupewe kikombe chetu, tumeanza kwa kishindo, tutamaliza kwa kishindo zaidi" imemalizia taarifa hiyo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI