Header Ads Widget

SIRRO ATAKA WAHITIMU TIA KUSAMBAZA UBUNIFU SHUGHULI ZA UCHUMI NA BAASHARA KIGOMA

 

Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro (wa pili kushoto) akikabidhi cheti na fedha kwa Mwanafunzi  Jasmin Hamisi aliyehitimu cheti cha awali cha uhasibu katika chuo cha uhasibu (TIA) Kampasi ya Kigoma ambaye alikuwa Mwanafunzi aliyefanya vizuri kitaaluma kwa wanafunzi wote wa ngazi ya Cheti waliomaliza chuoni hapo hivi karibuni.

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKUU wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro amewataka wahitimu wa kozi mbalimbali kutoka Taasisi ya  Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Kigoma kutumia elimu waliyopata kuisaidia jamii ya mkoa huo katika kufanya ubunifu na kusambaza ujuzi wa  usimamizi wa biashara ili  shughuli za kiuchumi zinazofanyika ziwe na tija kubwa.

Sirro alisema hayo wakati wa mahafali ya 23 ya TIA Kampasi ya Kigoma yaliyofanyika katika majengo mapya ya Kampasi hiyo yaliyo eneo la Kamara Kata ya Mngonya Halmashauri ya wilaya Kigoma mkoani Kigoma ambapo jumla ya wahitimu 756 walihitimu cheti cha awali na Diploma katika kozi mbalimbali za uhasibu, usimamizi wa rasilimali watu, ugavi na manunuzi.


Mkuu huyo wa mkoa Kigoma alisema kuwa kuwa muhitimu hiana maana ya kupata cheti lakini cheti hicho kitakuwa na thamani kama elimu iliyopatikana katika cheti hicho itatumika kuisaidia jamii hasa watu wa kipato cha chini walio wengi kufanya shughuli zao kwa tija na kuweza kuinua kipato chao.

 Alisema kuwa kwa sasa mkoa Kigoma unatekeleza Demokrasia ya uchumi kwa mkoa huo kuwa mkoa wa kimkakati kwenye masuala ya uchumi na biashara na kwamba pamoja na wawekezaji wakubwa na taasisi lakini wananchi wa kawaida wanayo nafasi kubwa kushiriki katika mpango huo hivyo wahitimu hao wanalo jukumu kubwa kusaidia ubunifu na usimamizi wa biashara na shughuli za kiuchumi za wananchi hao.


Akitoa taarifa kuhusiana na mahafali hayo Mtendaji Mkuu wa TIA,Profesa William Pallangyo alisema kuwa jumla ya wahitimu 756 wametunukiwa vyeti mbalimbali ambapo kati yao wahitimu wa cheti cha awali 262 ,Astashahada wakiwa 251 na Stashahada wapo 243.

Profesa Pallangyo alisema kuwa kuhitimu kwa wanafunzi hao kunalenga kujenga Tanzania iliyo bora inayopiga hatua mbele kimaendeleo katika kazi za ubunifu, usimamizi na utekelezaji wa shughuli za kiuchumi ambazo zitaleta mabadiliko makubwa kwenye Nyanja ya maendeleo kwa Watanzania.


Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro (katikati) akiingia kwenye ukumbi wa mahafali wakati w mahafali ya 23 ya Chuo cha Uhasibu (TIA)) Kampasi ya Kigoma ambapo wanafunzi 756 walimaliza kozi mbalimbali kwenye chuo hicho.

Wahitimu wa cheti cha awali cha mafunzo ya usimamizi wa biashara, rasilimali watu, ugavi, manunuzi kutoka TIA kampasi ya Kigoma

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI