Header Ads Widget

MBUNGE ABOOD AKABIDHI MADAWATI 526 KWA SHULE ZA MSINGI MOROGORO MJINI


Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Mohammed Abood amekabidhi jumla ya madawati 526 kwa shule kumi za msingi katika kata mbalimbali ndani ya jimbo hilo, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.

Shule zilizokabidhiwa madawati hayo ni pamoja na Mafisa B,  Misufini B, Mazimbu A, Chamwino B , Mawasiliano,  Kihonda -NOTTO, Sabasaba B, Tumaini na Area Five .

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mhe. Abood amesema hatua hiyo ni mwendelezo wa juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuhakikisha kuwa wanafunzi wanasoma katika mazingira bora na kuondokana na adha ya kukaa chini kutokana na uhaba wa madawati.

“Madawati haya ni sehemu ya dhamira ya Serikali yetu kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu katika mazingira rafiki. Mhe. Rais Samia ameweka nguvu kubwa katika sekta ya elimu, na sisi viongozi wa maeneo tunawajibika kuunga mkono jitihada hizo,” alisema Abood.

Aidha, Abood ameahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu ndani ya jimbo hilo, ikiwemo upungufu wa miundombinu mingine ya kufundishia na kujifunzia.

Kwa upande wao Wananchi pamoja na uongozi wa shule walimshukuru Mhe. Abood kwa mchango huo, wakieleza kuwa utapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa wanafunzi na kuongeza ufanisi wa utoaji elimu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI