Header Ads Widget

BREAKING:MOTO WAZULA BRAZIL UKUMBI WA MIKUTANO WAKIJADILI HALI YA HEWA

 


Na Matukio Daima Media 

TAHARUKI kubwa moto mkubwa ambao chanzo chake bado kufahamika  umezuka katika ukumbi wa mikutano unakoendelea mjadala wa hali ya hewa wa COP30 nchini Brazil, umesababisha washiriki kukimbia eneo hilo ili kujihami huku wengine 13 wakipatiwa matibabu kutokana na kuvuta moshi uliokuwa umetanda ikiwa bado siku mbili kabla ya kufungwa kwa mkutano huo.

Waandaaji wa mkutano huo Umoja wa Mataifa wamesema moto huo uliibuka jana Alhamisi Novemba 20, 2025, lakini ulidhibitiwa ndani ya dakika 6 na maofisa wa zimamoto, kisha waliamuru eneo lote la mkutano lifungwe kwa takriban saa 7 ili kufanya tathmini ya haraka.

Hata hivyo baadaye washiriki walianza kurejea katika eneo la mkutano wa COP30 baada ya kufunguliwa tena.

Wengine walirejea katika kumbi zilizo mbali na majengo ya pavilioni kuendelea na majadiliano huku wengine wakichukua mali walizoacha. Waziri wa Utalii wa Brazil, Celso Sabino, amewaambia waandishi wa habari katika eneo la tukio kwamba moto ulianzia karibu na Pavilioni ya China, mojawapo ya pavilioni nyingi zilizowekwa kwa ajili ya matukio ya pembeni ya mazungumzo ya hali ya hewa.


Gavana wa Jimbo la Pará, Helder Barbalho amekiambia kituo cha Habari cha G1 kwamba hitilafu ya jenereta au umeme katika kibanda huenda ndicho chanzo cha moto

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI