Header Ads Widget

WAUGUZI MBEYA WATAKIWA KUWAJALI WAGONJWA, LUGHA NZURI.

 

Na Josea Sinkala, Mbeya.

Huko mkoani Mbeya Muuguzi mkuu wa mkoa huo bi. Mhaza Mwanangwa, amekutana na wauguzi katika Halmashauri ya wilaya ya Mbeya na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu, nidhamu na kujali wagonjwa.

Akizungumza na wauguzi hao kwenye Hospitali ya wilaya ya Mbeya iliyoko Inyala, muuguzi mkuu wa mkoa wa Mbeya ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Mbeya chini ya mkurugenzi mtendaji Erica Yegella kwa usimamizi madhubuti katika kuhakikisha huduma za afya zinaendelea kutolewa ipasavyo na kuishukuru Serikali kuu kwa uboreshaji wa miundombinu ya huduma za afya na wataalam.
Akiteta na wataalam hao wa idara ya afya, bi. Mhaza amewataka kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa, kutowabagua kwa namna yoyote akisema Serikali ya Tanzania imeboresha miundombinu ya utolewaji huduma hiyo hivyo ni kazi ya wataalam kuhakikisha wanaendeleza kazi bora kwa wananchi wanaowahudumia.

Kwa upande wake muuguzi mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Nitike Kyejo, amesema Halmashauri ya Mbeya kwenye idara ya uuguzi watahakikisha wanazinganitia maagizo ya mkoa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

Nitike, amesema mara kadhaa wamekuwa wakifanya vikao na wauguzi wa maeneo mbalimbali katika eneo lao ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini za kila siku asubuhi kwa watumishi hao ili kujiridhisha na utendaji kazi wao.

Baadhi ya wananchi waliokuwa wakipata huduma kwenye Hospitali ya wilaya ya Mbeya wameishukuru Serikali kwa uboreshaji huduma na kupata matibabu vizuri huku nao wauguzi wakiahidi kuendelea kusimamia kanuni na maadili ya kazi yao ili kuendelea kuboresha utendaji kazi wao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI