Header Ads Widget

NJALU AAHIDI KUTOA MREJESHO WA AHADI ZAKE KILA BAADA YA MIEZI MITATU.

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Itilima, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Njalu Silanga akizungumza kwenye Mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Mahembe.


Na COSTANTINE MATHIAS, ITILIMA.


MGOMBEA Ubunge Jimbo la Itilima, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Njalu Silanga amesema kuwa endapo atachaguliwa Oktoba 29, 2025 atatia Mrejesho wa kilichofanywa kwenye ahadi zake anazozitoa sasa kila baada miezi mitatu.


Akizungumza kwenye mikutano ya kampeni katika vijiji vya Kilugala, Mwamnemha, Mahembe, Isengwa na  Sasago ikiwa ni mwendelezo wa mikutano ya kampeni kijiji kwa kijiji kutafuta kura za Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge na madiwani wa CCM.


Amesema endapo atapewa ridhaa atahakikisha anatoa mrejesho kila baada ya miezi mitatu juu ya Utekelezaji wa ahadi anazotoa ambazo zinahusiana na Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2025/2030.



"Kama ambavyo tumekuja leo kuomba kura ndivyo ambavyo tutakuja hata baada ya uchaguzi kwakua tuna nia ya dhati ya kuijenga Itilima yetu na tumejipanga kufanya tathimini ya utekelezaji wa ahadi kila baada ya miezi mitatu ili kuwapa mrejesho kipi tumeahidi na hatua zake za utekelezaji" amesema Njalu.


mwisho. 




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI