Abas ni mtoto wa mstaafu Marehemu Ali Hassan Mwinyi Abbas Mwinyi ambae ni kaka wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mwinyi Leo Septemba 25 amefariki Dunia akiwa Hospitali ya Lumumba Mjini Unguja
Abbas Mwinyi ni mtoto wa Mstaafu Mzee Mwinyi ambae kabla ya umauti wake alikua msemaji wa familia maara Baada kifo cha mzee
Abbas alikua Mbunge wa Fuoni Zanzibar kwa Muhula uliokwisha mbapo hivi sasa alikua akitetea nafasi hiyo kupitia CCM.
T A A R I F A Y A M A Z I K O
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt Hussein Ali Hassan Mwinyi anasikitika kutangaza kifo cha Kaka yake Rubani Abbas Ali Hassan Mwinyi aliyefariki leo, Alhamis Tarehe 25 Septemba 2025 Jijini Zanzibar..
Ibada ya kumsalia Marehemu itafanyika katika Msikiti wa Zanzibar ( جميع ) - *Msikiti wa Qaboos baada ya sala ya Ijumaa na baada ya hapo maziko yanafanyika Mangapwani katika eneo ambalo amezikwa Mzee Ali Hassan Mwinyi* - ambapo watu waliopo maeneo ya Mangapwani, Bumbwini, Fujoni na maeneo ya karibu watapata kutabaruku kabla ya kuzika.
Visomo Msikitini vitaanza saa 4 asubuhi.
*إنا لله وانا إليه راجعون*








0 Comments