Header Ads Widget

SHULE ZATAKIWA KUZINGATIA MTAALA MPYA WA ELIMU ULIOBORESHWA.

 

Na Mwandishi Wetu Matukio Daima App Kibaha

IDARA ya Udhibiti Ubora wa Elimu Manispaa ya Kibaha inaendelea kutoa semina elekezi kwa walimu wa shule binafsi ili wazingatie mtaala mpya wa elimu ulioboreshwa.

Hayo yalisemwa na Ofisa Udhibiti Ubora wa Manispaa ya Kibaha Asha Kiliza wakati wa mahafali ya pili ya wanafunzi wa darasa la awali kwenye shule ya awali na msingi ya Finest iliyopo Kibaha.

Kiliza alisema kuwa semina hizo ni endelevu ambazo hutolewa kwa walimu wa shule hizo ili wafuate miongozo mbalimbali inayotolewa na wizara ili kutoa elimu bora.

"Tumekuwa tukitoa semina elekezi kwa shule binafsi ili wazingatie mtaala wa elimu ulioboreshwa ambao unaoendana na hali halisi ya sasa ili kuwa na elimu bora ambayo itamwezesha mwanafunzi kupata elimu bora,"alisema Kiliza.

Awali mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo ya mchepuo wa Kiingereza ya Finest Profesa Mrisho Malipula alisema kuwa mipango yao ni kuongeza vyumba vya nadarasa zaidi.

Malipula alisema kuwa baadhi ya changamoto ni miundombinu ya barabara kutôkuwa rafiki hasa kipindi cha mvua ambapo magari ya shule huharibika sana na aliwaomba wazazi kulipa ada kwa wakati ili kufanikisha mipango mbalimbali ya shule na kufuatilia maendeleo yao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI