Header Ads Widget

BODABODA, WAFANYABIASHARA WAITWA KUMPIGIA KURA DK. SAMIA.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Bariadi Mjini kupitia CCM, Mhandisi Kundo Mathew, akinadi sera na kuomba kura kwa wananchi.


Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Bariadi Mjini kupitia CCM,  Mhandisi Kundo Mathew, amewataka vijana wanaondesha Bodaboda (almaarufu Maafisa Usafirishaji) pamoja na Wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kumpigia kura za Kishindo Mgombea Urais Dk. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kutatua changamoto zao.


Mhanidisi Kundo amesema kuwa katika miaka minne ya Utawala wa Rais Dk. Samia, serikali imethibiti na kushusha bei Mafuta ili kuleta ahueni ya maisha kwa Bodaboda, Wafanyabiashara na wananchi wa kawaida.


Akizungumza kwenye mikutano ya kampeni iliyofanyika katika Mitaa ya Shimbale (kata ya Mhango) na Nyakabindi (kata ya Nyakabindi), Mhanidisi Kundo amesema kuwa licha ya kuwepo vita ya Urusi na Ukraine, Serikali ya Dk. Samia imedhibiti mfumuko wa Bei ya mafuta ili kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji.




"Miaka minne ya serikali ya Rais Dk. Samia imedhibiti mfumuko wa Bei ya mafuta, wafanyabiashara na Bodaboda wamefurahi hata wananchi wamefurahi sababu gharama za usafiri zilizokuwa zimepanda, Sasa zimeshuka...Tumpigie kura Dk. Samia sababu ameshusha bei ya mafuta, ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa mazao na bidhaa" amesema Mhandisi Kundo.


Amesema kuwa serikali ya Rais Dk. Samia imeweka ruzuku ya Mafuta ili wananchi ili ili wapate huduma inayoenda na kipato chao, hivyo wanapaswa kumpigia kura Mgombea Urais ili aendelee kuwahudumia wananchi.


Mwisho.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI