Header Ads Widget

WANANCHI WAMEJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

Wananchi wamejitokeza kwa wingi katika Kituo cha Kupigia Kura cha Kariakoo, Jimbo la Kwahani leo Jumatano, Oktoba 29, 2025 kushiriki katika Uchaguzi Mkuu. 

Foleni ndefu zimeonekana mapema asubuhi huku wakazi wa maeneo mbalimbali wakionekana na hamasa kubwa ya kutimiza haki yao ya kikatiba.


Katika uchaguzi huu, Wazanzibari wanapata fursa ya kupiga kura tano za kuwachagua Rais wa Zanzibar, Wabunge, Wawakilishi, Madiwani pamoja na Diwani wa Viti Maalum, hatua muhimu katika kuamua mustakabali wa uongozi wa Taifa kwa miaka ijayo.


Muda mfupi kutoka sasa Mgombea wa Urais wa Zanzibar anatarajia Kupiga kura katika Kituo hicho.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI