MKUU wa Wilaya ya Bariadi, Mkoani Simiyu, Simon Simalenga (mwenye koti na tisheti nyekundu) akikata utepe kwenye uwekezaji wa jiwe la msingi kituo cha Afya kilalo.Na SAKAGOI KAPAGALA, Bariadi.
MKUU wa Wilaya ya Bariadi, Mkoani Simiyu, Simon Simalenga amewaka jiwe la msingi katika kituo cha Afya kilichopo Kijiji cha Kilalo wilaya ya Bariadi Mkoani humo.
Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi, Simalenga amesema kuwa kituo hicho kitasogeza huduma ya Afya na Matibabu kwa wananchi ambao walikuwa wakitembea mwendo mrefu kwenda kituo cha Afya Ngulyati kilichopo Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
MKUU wa Wilaya ya Bariadi, Mkoani Simiyu, Simon Simalenga (kulia) akifungua kitambaa wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa kituo cha Afya Kilalo."Awali kituo hiki kilikuwa na mtoa huduma mmoja, Rais Dkt. Samia aliposikia tunakuja kuweka jiwe la msingi hapa, ametuongezea watumishi wawili na Sasa wamefikia watatu...tuendelee kuiunga mkono serikali sababu inatusogezea huduma karibu na maeneo yetu" amesema Simalenga.
Maria Lucas mkazi wa kilalo amepongeza ujenzi wa kituo hicho ambao umesogeza huduma ya matibabu kwa wananchi hao kwani awali walikuwa wanahangaika kupata huduma hususani mama wajawazito na watoto.
Juma Magi, mkazi wa kilalo amesema wakina mama na watoto walikuwa wanapoteza maisha kutokana na kukosa huduma ya matibabu karibu na maeneo yao na kwamba baada kituo hicho kujengwa wamesogezewa huduma ya matibabu.
Hadi kukamilika Kwa kituo hicho linatarajia kugharimi kiaos Cha shilingi Mil. 600 ambapo hadi Sasa serikali imetoa kiasi cha shilingi Mil. 250 Kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), kichomea taka pamoja na matundu matano ya vyoo.
Mwisho.









0 Comments