Header Ads Widget

WANANCHI WAANZA KUPIGA KURA MJINI BARIADI.

 



Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


ZOEZO la Upigaji kura limeanza katika vituo mbalimbali mjini Bariadi Mkoani Simiyu, huku wananchi wakijitokeza tangu mapema kupiga kura.


Kulingana na utaratibu uliowekwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi katika mpangilio wa Majina kwa herufi na kuwepo vituo vingi vya kupigia kura ili kurahisisha zoezi hilo linaloendelea nchi nzima.


Wakizungumza na waandishi wa Habari, wananchi waliofika kupiga kura akiwemo Ernest Mapinda wameipongeza serikali kwa kuandaa Mazingira rafiki na salama ya kupigia kura.




Kwa Mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bariadi Mjini Oswald Rwezahula, ameeleza kuwa Jimbo hilo lina vituo 327 na wapiga kura 123,332.


Naye Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bariadi vijijini, Beatrice Gwamagobe amesema kuwa Jimbo hilo lina vituo  493 na wapiga kura 195,049.


Mwisho.













Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI