NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
SPIKA wa Bunge ambaye pia ni mgombea wa Jimbo la Uyole, Dkt. Tulia Ackson, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa amani na utulivu, akisisitiza umuhimu wa kutumia haki yao ya kidomokrasia kuchagua viongozi wanaowataka.
Dkt. Tulia alitoa wito huo mara baada ya kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Tambukareli, ambako aliwasihi wananchi wasikae majumbani bali washiriki kikamilifu katika zoezi hilo muhimu kwa mustakabali wa taifa.
Amesema uchaguzi ni fursa ya wananchi kuamua mustakabali wa nchi yao kupitia kura, hivyo ni wajibu wa kila mwenye sifa kuhakikisha anatumia haki hiyo kwa utulivu na uwajibikaji.
Aidha, amewapongeza watendaji wa tume ya uchaguzi kwa maandalizi mazuri na kuhimiza kuendelea kudumisha amani wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi.






0 Comments