Na Mariam Kagenda ,Matukio Daima Media, Kagera
Wananchi wa Jimbo la Ngara mkoani Kagera wamehimizwa kuendelea kulinda amani iliyopo kwani amani ndo msingi mkubwa wa maendeleo
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ngara kupitia Chama cha Mapinduzi Bwana Dotto Jasson Bahemu amewakumbusha wakazi wa Jimbo hilo kutambua kuwa Amani ndio nguzo kubwa ya maendeleo ya taifa.
Bw Dotto Bahemu amesema hayo kwenye mkutano wake wa kampeni ikiwa ni mwendelezo wa mikutano hiyo yenye lengo la kuomba Ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo
Amesema utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoahidiwa kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) unategemea amani na utulivu wa taifa wakati na baada ya uchaguzi.
Bw Dotto Bahemu amewasisitiza wakazi wa Jimbo la Ngara kukumbuka athari za kuvurugika Kwa Amani na Usalama kwenye Mataifa jirani hivyo hawatakiwi kuvuruga amani iliyopo .

Ameongeza kwamba wakazi wa Ngara hawatakiwi kushiriki katika vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani kwani hata baada ya Uchaguzi wanatakiwa kubaki salama .
0 Comments