Header Ads Widget

MKUU WA MKOA KAGERA AHAMASISHA VIJANA KIFANIKISHA NDOTO KUPITIA KONGANI.

 

Na Shemsa Mussa -Matukio Daima Media 

Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Bi. Hajjat Fatma Mwassa, amekutana na kuzungumza na vijana wanaofanya kazi katika kongani ya vijana ya Manispaa ya Bukoba, ambapo amesisitiza dhamira ya Serikali kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana, hususan katika eneo la upatikanaji wa ajira.

Akizungumza katika ziara hiyo, Bi. Mwassa amesema Serikali imeendelea kutoa fursa za ajira zisizo rasmi kwa vijana kupitia miradi inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo,amesema Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara, bandari na mradi wa bomba la mafuta unaopita katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Kagera.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kushirikiana na taasisi kama VETA ili kuwapatia vijana mafunzo ya ufundi stadi yanayowasaidia kupata ajira na kipato, sambamba na kuwawezesha kuwa wabunifu katika kubuni vyanzo mbalimbali vya kujitegemea. 

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa ameahidi kuwa Serikali itaendelea kutoa msaada wa vifaa muhimu kwa ajili ya kuimarisha kongani hiyo ya vijana, huku akitoa wito kwa vijana kufanya kazi kwa bidii bila kujihusisha na makundi yasiyokuwa na tija kwa maendeleo yao.

 “Ndoto yangu ni kuwaona mnapata faida ya kweli na ya kudumu kupitia kongani hii. Natamani siku nikistaafu nije kutembelea hapa na nionekane miongoni mwa watu mnaonitunukia zawadi kwa tabasamu kubwa la mafanikio ” amesema Bi. Mwassa.

Mpaka sasa jumla ya vijana 70 wanaendelea kupata mafunzo na maarifa kupitia kongani Kwa fani na ujuzi mbalimbbali .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI