Header Ads Widget

MFUMO WA UGAWAJI MBEGU KIDIGITALI KUONDOA MALALAMIKO KWA WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA KISHAPU.

 

Afisa Kilimo kutoka Bodi ya Pamba Wilaya ya Kishapu Joachim Gobanya akizungumzia upotevu wa mbegu za pamba uliokuwepo kutokana na wakulima kutumia mbegu za pamba Kwa matumizi yasiyo sahihi kabla ya mfumo wa ugawaji mbegu kidigitali kuwafikia.
Afisa Kilimo  BBT, kutoka Kijiji Cha Masanga Grace puleleamesema   akizungumza ugawaji wa mbegu kidigitali umeimarisha uwajibikaji katika ugawaji wa mbegu Kwa wakulima.
Katibu wa AMCROSS ya Masanga Mkumbo mashishanga akizungumza mfumo wa ugawaji mbeguza pamba kidigitali utakavyowasadia kuondoa udanganyifu Kwa wakulima kuchukua mbegu Kwa kujirudia

Na Chausiku Said 

Matukio Daima 

Mfumo wa ugawaji wa mbegu za pamba kidijitali umeelezwa kuwa suluhisho la kudumu katika kuhakikisha wakulima wanapata mbegu kwa haki, uwazi pamoja na kudhibiti udanganyifu wa upotevu wa mbegu na kuondoa changamoto za wakulima kuchukua mbegu Kwa kujirudia

Kupitia mfumo huo wa kidijitali umeondoa changamoto ya wakulima kudanganya ukubwa wa mashamba waliyonayo, pia viongozi na wataalamu wa kilimo wana uwezo wa kubaini taarifa halisi za mkulima, ikiwemo idadi ya hekari alizonazo, kijiji anachotoka na kiasi cha mbegu anachostahili kupewa.

Kwa mujibu wa viongozi wa AMCROSS, Wilaya ya kishapu Mkoani Shinyanga , wameeleza kuwa mfumo huo umewawezesha wakulima kujiridhisha kiasi cha mbegu anachostahili kupokea kulingana na hekari alizosajili kwenye mfumo, huku mfumo huo ukidhibiti tabia ya baadhi ya wakulima kuchukua mbegu na kwenda kuuza

Katibu wa AMCROSS ya Masanga Mkumbo mashishanga ameeleza kuwa kupitia mfumo huo wanaweza kumtambua mkulima anahitaji kiasi gani Cha mbegu na ugawaji wa mbegu hizo unazingatia usawa kulingana na ukubwa wa shamba na lakini pia ili mkulima aweze kupata mbegu za ruzuku anapaswa kuwa na namba ya mkulima na namba ya simu aliyosajiliwa kupitia mfumo.

"Mkulima anaposajiliwa kwenye mfumo, hupata namba ya siri inayohusishwa na namba ya simu aliyosajiliwa, jambo linalomwezesha mkulima kupata mbegu za ruzuku bila usumbufu, lakini pia sisi kama viongozi tunawajua watu wetu, hivyo mfumo huu umetupa uwezo wa kufahamu kama mkulima amelimbikiza hekari na kumpa mbegu kulingana na hali yake halisi,” amesema Mashishanga.

Afisa Kilimo  BBT, kutoka Kijiji Cha Masanga Grace puleleamesema kuwa  mfumo huo umeimarisha uwajibikaji katika ugawaji wa mbegu, kwani kila mkulima huhudumiwa mmoja mmoja huku taarifa zake zikirekodiwa lakini Kabla ya mfumo huu, kulikuwa na changamoto ya wakulima kujirudia kuchukua mbegu kwa kutumia vitambulisho tofauti.

 “kwa kutumia mfumo huu wa ugawaji mbegu kidigitali umetusaidia kufahamu mkulima amechukua mifuko mingapi ya mbegu na analima hekari ngapi, jambo ambalo linatusaidia kumfuatilia na kuhakikisha anatumia mbegu kwa malengo ya kilimo,” amesema Pulele.

Afisa Kilimo kutoka Bodi ya Pamba Wilaya ya Kishapu Joachim Gobanya ameeleza kuwa kulikuwa na upotevu wa pembejeo kutokana na wakulima kutumia mbegu za pamba Kwa matumizi yasiyo sahihi ikiwemo kulisha mifugo, kukamua mafuta pamoja na kuuza badala ya kwenda kupanda.

"Kwa hiyo mfumo wa kidigitali utatusadia kufahamu ni mkulima yupi kapata mbegu na amepata kulingana na hekari alizoandikana na wakati wa kupewa mbegu hizi lazima tufahamu hekari alizosajili na anapokuwa amechukua mbegu lazima na sisi tuwe na taarifa zake "Alisema Gobanya.

Gobanya ameeleza kuwa bodi ya pamba tayari imetoa tani 73 za mbegu ambazo ni lazima zigaiwe Kwa mfumo wa kidigitali, kwani mfumo huu ni maelekezo ya serikali kuwa pembejeo zote zinazohusiana na kilimo zinagaiwe Kwa njia ya ruzuku, ili kujua kama ruzuku inawafikia wakulima.

"ndio maana serikali ikaje na mfumo huu wa kidigitali, tukiwa na mfumo wa kidigitali tutaweza kutambua wakulima waliopata pembe jeo ni wakulima wangapi na kutambua Wana mashamba yenye ukubwa kiasi gani na maeneo wanayoishi kupitia namba za wakulima ambazo wanazitumia wakati wa kupokea pembejeo hizo"Alisema Gobanya.

Mkulima kutoka Kijiji Cha Mwampalo Phabian Mgoma,  ameishukru bodi ya pamba kuja na mfumo huo wa  ugawaji mbegu kidigitali kwani utasaidia sana wakulima kupata mbegu bila kuwa na malalamiko tofauti na nyuma, na tunapata mbegu Kwa wakati.

 "Awali, mtu alikuwa anadanganya ana hekari 50, apewa mifuko 30, anauza 20 na anabakiwa na mifuko 10 lakini Sasa hivi anapewa kulingana na alivyosajili, Mfumo huu ni rafiki kwa wakulima," alisema Mgoma.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI