NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
DODOMA.Wananchi wa Jimbo la Kondoa Vijijini, mkoani Dodoma, leo tarehe 29 Oktoba 2025, wamejitokeza kwa wingi na kupanga foleni katika Kituo cha Stendi ya Zamani kushiriki zoezi la kupiga kura ya kumchagua Rais, Mbunge na Diwani.
Ushiriki huo unaonyesha dhamira ya Watanzania kutimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Zoezi la upigaji kura linaendelea kwa amani na utulivu katika maeneo mbalimbali nchini, huku wananchi wakionekana na hamasa kubwa katika kutekeleza wajibu wao wa kiraia.

.jpeg)






0 Comments