NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
IRINGA.Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Salim Abri Asas amepiga kura mapema leo katika Kituo cha Chuo cha Afya 1, Manispaa ya Iringa na kueleza kuwa zoezi la kupiga kura limeanza kwa utulivu na amani kubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupiga kura Asas amesema kuwa yeye pamoja na wananchi wengine tayari wametimiza wajibu wao wa kikatiba na kusema kwa ufupi, “Tayari tumetiki.”
Ameongeza kuwa hali ya utulivu na amani imetawala katika Manispaa ya Iringa na Mkoa kwa ujumla, jambo linalodhihirisha uimara wa demokrasia na umoja wa Watanzania.
“Asas” amesisitiza kuwa uchaguzi huu ni miongoni mwa chaguzi zenye historia kubwa ya amani nchini tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, na anaamini utahitimishwa kwa mafanikio makubwa na utulivu wa kipekee.
MWISHO.








0 Comments