Header Ads Widget

MKUU WA MKOA WA IRINGA ASHIRIKI ZOEZI LA KUPIGA KURA

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

IRINGA.Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, mara baada ya kumaliza haki yake ya kikatiba ya kupiga kura katika Kituo cha Kinondoni Flat 2, amezungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa zoezi la kupiga kura limeanza vizuri huku wananchi wakijitokeza kwa wingi.

Amesema hali ya usalama katika vituo vyote vya kupigia kura ni shwari na maandalizi yamekuwa mazuri, hivyo wananchi waendelee kujitokeza kutumia haki yao ya msingi.

Kheri James amesisitiza kuwa kura zitahesabiwa kwa usalama na matokeo kutangazwa kwa utulivu, huku akiwataka wananchi kuepuka vitendo au maneno vinavyoweza kuvuruga amani.



Aidha, amepongeza wananchi waliopiga kura mapema na kuwataka wengine kufuata mfano huo, akisisitiza kuwa muda bado unaruhusu ili kila mmoja atimize wajibu wake wa kikatiba.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI