Header Ads Widget

WANANCHI WA KIJIJI CHA OLPIRO WILAYANI NGORONGORO WANUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI SAFI YA UHAKIKA.


Na,Jusline Marco:Arusha

Wananchi wa Kijiji cha Olpiro kilichopo katika Kata ya Eyasi Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha wamefanikiwa kupata huduma ya maji safi na salama baada ya Mamlaka ya hifadhi eneo  la Ngorongoro kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii  kutembelea kijiji hicho na kuchukua hatua za kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi pamoja na mifugo yao.

Wataalam kutoka NCAA wakiwa katika ziara yao, wameweza kukagua marekebisho na ukarabati wa miundombinu ya maji uliofanyika katika kijiji hicho, ambapo ukarabati wa miundombinu  ya huduma ya maji katika kijiji hicho umeleta faraja kubwa kwa wananchi hao ambao waliokuwa wakikabiliwa na changamoto ya uhaba wa maji kwa muda mrefu.

Aidha katika maboresho ya huduma ya maji,Mamlaka hiyo pia imefanya tathmini ya miundombinu mingine ikiwemo josho la kuogeshea mifugo lililopo katika kijiji hicho.

Nao Wananchi wa kijiji cha Olpiro wameipongeza Serikali kupitia Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa jitihada hizo wakieleza kuwa zinachangia sio tu katika kuboresha maisha yao ya kila siku bali kulinda afya zao na kuendelea kuunga mkono Serikali katika  shughuli za uhifadhi.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI